Madaktari Embu watisha kugoma
Na George Munene
Madaktari wa Kaunti ya Embu wametishia kugoma kutokana na mazingira duni ya kufanyia kazi. Walipeana notisi ya siku saba kwa Gavana Martin Wambora ambaye walimlaumu kwa kufumbia mahangaiko yao.
Wakiongozwa na katibu wa KMPDU Elvis Mwandiki, zaidi ya madaktari 80 walisema kwamba hawajapokea mshahara wao wa miezi miwili iliyopita.
Wataalamu hao waliseema kwamba hawajawaipokea marurupu ya corona na walifukuzwa walimokuwa wakiishi kwasababu ya kutolipa kodi ya nyumba.
Madakatri hao walilia kwamba hakuwa wamelipa kodi ya nyumba na kwamba wenye nyumba walikuwa wanatishia kuwafukuza.
“Wenzetu wanapitia mambo magumu kwasababu hawajakuwa wakipokea pesa zao,” alisema Bw Mwandiki.
Waliilaumu pia serikali ya kaunti hiyo kwa kutowapa vifaa vya kujikinga na virusi vya corona.
Madaktari hao waliapa kukatiza shughuli za matibabu kama malalamiko yao hayatashughulikiwa.
Tafsiri na Faustine Ngila