Madaktari wengine wafariki kutokana na corona
Na CHARLES WASONGA
MADAKTARI wawili ni miongoni mwa watu 21 waliothibitishwa kufariki kutokana na Covid-19 ndani ya saa 24 zilizopita, Wizara ya Afya ilithibitisha Jumamosi. Idadi hii inafikisha 1, 249 idadi jumla ya vifo kutokana na ugonjwa huu tangu ulipolipuka nchini mnamo Machi 13, 2020.
Kwenye taarifa aliyoituma kwa vyombo vya habari Waziri Mutahi Kagwe alisema kuwa watu 1,080 walipatikana na virusi vya corona baada ya sampuli kutoka watu 8,322 kupimwa.
Hii ina maana kuwa kufikia Jumamosi, Novemba 14, 2020, Kenya imeandikisha idadi jumla ya maambukiza ya watu 69,273.
Miongoni mwa wagonjwa hao 1,080 wapya 216 wanatoka Nairobi, Mombasa (163), Nakuru (103), Kilifi (64), Baringo (60), Machakos (57), Kisumu (56), Bungoma (41), Uasin Gishu (41), Kiambu (30), Turkana (30) na Migori 28,
Katika kaunti ya Busia watu 23 walipatikana na virusi vya corona, Kajiado (21), Kakamega (20), Kisii (18), Kericho (16), Nyamira (16), Nandi (15), Nyeri (12), Tharaka Nithi (12), Meru (8), Trans Nzoia (8), Siaya (5), Samburu (4,) Narok (3).
Kaunti zifuatazo nazo ziliandikisha kisa kimoja kila moja;, Kirinyaga , Taita Taveta , Laikipia, Murang’a, Nyandarua, Vihiga Kwale, Wajir , Elgeyo Marakwet na Bomet.
Waziri CS Kagwe pia alisema kuwa wagonjwa 542 walipona- 262 kutoka mpango wa utunzaji nyumbani na 280 waliokuwa wamelazwa katika hospitali mbali mbali nchini.
Kwa hivyo, kufikia Jumamosi idadi jumla ya wagonjwa ambao wamepona nchini na kurejelea maisha yao ya kawaida ni 45, 414.
“Vile vile jumla ya wagonjwa 1,185 wamelazwa katika hospitali mbalimbali nchini wakitibiwa corona ilhali wengine 5,794 wanatunzwa nyumbani,” akasema taarifa hiyo.
Ikaongeza: “Miongoni mwao, wagonjwa 58 wako katika vyumba vya wagonjwa mahututi ilhali 23 watasaidia kupumua na 30 wanaongezewa oksjeni.”