Madiwani wazidi kumenyana na Waiguru
GEORGE MUNENE na FAUSTINE NGILA
Vita dhidi ya madiwani wa kaunti ya Kirinyaga na Gavana wa kaunti hiyo Anne Mumbi Waiguru bado vinaendelea.
Madiwani hao wanatishia kwenda kwenye mahakama ya juu kuhusiana na maamuzi ya maseneta ya kumuokoa gavana waiguru kutokana na kutolewa mamlakani.
Kupitia diwani Ndegwa Njiru madiwani wa hao 23 walipiga kura ya kumtoa malaknai Bi Waiguru kwenye mswada uliogozwa na Kinyua Wangui diwani wa Mutira walisema kwamba hawakutotesha na uamuzi wa maseneta.
Madiwani hao walipuuzilia mbali ripoti ya kamati hiyo kwamba njia waliyotumia kumtoa mamlakani Bi Waiguru haikufaa.
“Wateja wangu hawakufurahishwa na uamuzi uliotolewa na kamati ya seneti na itawalazimu waende kortini kutafuta hali,” alisema Bi Njiru .
Mwanasheria huyo alisema kwamba madiwani na Wakenya walishangazwa na uamuzi wa kamati hio.
“Tuliipa seneti ushaidi wa kutosha wa kuonyesha kwamba gavana huyo hafai kuwa ofisi lakini seneti ilipuuzilia mbali ushaidi huyo na wakansafisha .Seneti imetutudisha nyuma kwenye vita ya kuakikisha kwamba kuna demokrasia,’’ alisema Bw Njiru.
Madiwani hao walisema kwamba vita vyao na gavana Bi Waiguru viko mbali kuisha.
Hii inajiri baada ya Bi Waiguru kuwasamehe madiwani waliokuwa wamemng’oa.