Habari Mseto

Mafuriko yatatiza uchukuzi Homa Bay

November 16th, 2020 Kusoma ni dakika: 1

GEORGE ODIWUOR NA FAUSTINE NGILA

Usafiri kwenye barabara ya Homabay – Katito ulisitishwa kwa saa kadhaa Jumatatu baada ya mto kuvunja kingo zake.

Magari yalikuwa yamekwamba kwa muda wa masaa matano karibu karibu na soko la Nyangweso baada ya mafuriko kufunikia daraja la Awach Tende.

Wakazi wa Nyaluny, Tethra na Kijiji cha Nyarut walilazimika kuhama kufuatia mafuriko hayo. Vijana kutoka Kijiji hicho cha walichukua faida ya mafuriko hayo na kusukuma magari na kulipwa 200 na 500.

Magari ya uchukuzi ya umma yalitumia njia zingine kupitia Kijiji cha Rangwe ili kufika maeneo yao

Bw Capis Otieno dereva wa matatu alisema kwamba aliwarudishia abiria pesa yao baada ya kukwamba.

“Nitaenda nyumbani bila pesa kwani mipango yangu yote imeharibika kwasababu abiria ambao nilikuwa nipeleke Kisumu wametka kwa gari na wakaabiri gari nyingine.Singehatarisha Maisha yangu kwa kuvuka mto huo nikiwa na abiria hao,”Wakazi wameomba serikali ijenge binu za kuzuia mafuriko.

Bi Nereah Ochanda mkazi alisema kwamba alipoteza kuku wake wote kwa sababu ya mafuriko.

“Niliamka saa kumi asubuhi nikapata nyumba yangu imeejaa maji.Hii ndio imekuwa mtindo wa kwa miak mingi.Serikali inapaswa kutafuta suluhu ya shida hizi,”alisema.