Habari Mseto

Mafuta yapungua kwa kwa Sh9

January 15th, 2019 Kusoma ni dakika: 1

Na WANDERI KAMAU

WAKENYA watapata afueni kwa mwezi mmoja ujao baada ya Halmashauri ya Kudhibiti Kawi Kenya (ERC) kupunguza bei ya mafuta.

Kulingana na bei mpya zilizotangazwa na halmashauri hiyo jana, bei ya petroli jijini Nairobi itagharimuSh104.21 kutoka bei Sh113.54.

Watumizi ya dizeli watalipa Sh102.24 kutoka Sh112.28, huku watumizi wa mafuta taa wakilipa Sh101.70 kutoka Sh105.22.

Jijini Mombasa, watumizi wa petroli watalipa Sh101.60, dizeli Sh99.63 nao watumizi wa mafuta taa wakilipa Sh99.09 kutoka wastani wa Sh105 mwezi uliopita.

Jijini Kisumu, Wakenya watalipa Sh105.73 kwa lita moja ya petroli, Sh103. 94 kwa dizeli na Sh103.40 kwa lita moja ya mafuta taa.

Hii ni afueni kubwa kwa Wakenya, hasa baada ya Rais Uhuru Kanyatta kutia saini Mswada wa Fedha 2018, ambao unapendekeza ushuru wa asilimia nane kwa mafuta na bidhaa zinazotengenezwa kutokana nayo.

Rais Kenyatta alilazimika kupunguza asilimia hiyo kutoka asilimia 16, baada ya Wakenya kulalamikia bei ghali ya huduma muhimu kama usafiri.

Kwenye mpango huo, serikali inalenga kupata fedha za kuimarisha miundomsingi.