• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 12:11 PM
Mahakama yakataa wahasibu wakitimuliwa kazini

Mahakama yakataa wahasibu wakitimuliwa kazini

Na RICHARD MUNGUTI

MAHAKAMA ya kushugulikia kesi za mizozo ya wafanyakazi (ELRC) illkataa kufutilia mbali agizo ya iliyotoa wiki iliyopita ikisitisha barua ya kuwatimua kazi wahasibu.

Jaji Onesmus Makau (pichani) alikataa kufuta agizo aliyotoa na kuamuru kesi iendelee Jumatano.

Serikali iliomba korti itupilie maagizo ya kusitisha kuhojiwa upya kwa wahasibu na wasimamizi wakuu wa idara za ununuzi wa bidhaa yaliyotolewa na Rais Uhuru Kenyatta na kutekelezwa na mkuu wa utumishi wa umma Bw Joseph Kinyua.

Na wakati huo huo Jaji Onesmus Makau alikataa kusitisha utekelezaji wa agizo la Bw Kinyua hadi kesho kesi itakaposikizwa.

Akiwasilisha ombi la kuondoa agizo hilo, Jaji Makau alielezwa na wakili mkuu wa Serikali Bw Kennedy Ogeto kuwa kuachiwa ofisi kwa manaibu wa wakuu hawa hakumaanishi wamefutwa kazi, “La hasha.”

Mahakama iliambiwa hatua hiyo ilichukuliwa katika jitihada mpya za Rais Kenyatta kufagia ufisadi Serikalini.

Mwanaharakati Okiya Omtatah akiwa kortini katika kesi ya kuwatimua wahasibu. Picha/ Richard Munguti

Jaji Makau aliambiwa baada ya kuhojiwa haya mapya watakaofaulu watarudishwa kazini.

“ Kinachoendelea serikalini sasa sio ufisadi mbali ni uporaji mtupu.Mmoja hawezi kupata huduma serikali hadi atakapochomoa mabunda ya pesa kutumikiwa,” alisema wakili George Oraro anayemwakilisha mwanasheria mkuu na Bw Kinyua.

Bw Oraro alimweleza Jaji Makau kuwa Tume ya kuajiri Watumishi wa Umma (PSC) iliyoshtakiwa pia na Bw Omtatah bado haijawasilisha ushahidi wake na msimamo wake ni kesi ya Bw Omtatah ifutiliwe mbali.

Bw Oraro alisema Bw Omtatah hakuelezea korti ukweli jinsi ulivyo kuhusu agizo hilo kwamba wahasiriwa hawajaachishwa kazi mbali watakuwa wanapokea mishahara.

Mwanaharakati huyu alikuwa amepotosha korti akidai Bw Kinyua sio mkuu wa utumishi wa umma.

“ Mlalamishi hakufichulia korti amemshtaki Bw Kinyua katika kesi nyingine itakayoamuliwa Juni 22 2018. Bw Omtatah amemshtaki Bw Kinyua kwa kufutilia mbali muda uliowekwa wa watumishi wa umma kustaafu wakitimisha umri wa miaka 60, ” alisema  Bw Oraro.

Bw Omtatah alipinga ombi hilo akisema Serikali inataka kutumia njia ya mkato kuzamisha kesi hiyo ambapo anasema Bw Kinyua hana mamlaka ya kuwasimamisha kazi wahasibu na wakuu wa idara za kununua mali ya umma.

You can share this post!

Polisi pabaya kwa mauaji ya mwanamke City Park

Uamuzi kuhusu dhamana kwa washukiwa 47 wa NYS kutolewa Juni...

adminleo