• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 3:42 PM
Mahakama yakubali maafisa wa Kitui washtakiwe

Mahakama yakubali maafisa wa Kitui washtakiwe

Na RICHARD MUNGUTI

MAHAKAMA ya Kuamua Mizozo ya Wafanyakazi (ELRC) imekubalia maafisa wawili wakuu katika kaunti ya Kitui  washtakiwe kwa kukaidi maagizo ya mahakama.

Mabw  Joshua Nyamai Mutembei na Sammy Musau walikubaliwa na Jaji Maureen Onyango kuwashtaki Mabw Japheth Mbiti na Alex Kimanzi kwa kukaidi agizo wasitimuliwe kazini.

Wawili hao walikuwa wameishtaki kaunti ya Kitui na bodi ya utenda kazi.

Makamama ilikuwa imewaamuru wawili hao wasiwape kazi nyingine wawili hao lakini wakamwamisha Bw Mutembei kutekeleza majukumu yasiyokubaliwa.

Katika kesi aliyowashtaki Mabw Mbiti na Bw Kimanzi  mlalamishi amesema kuwa wawili hao walikaidi agizo Jaji Onyango kwa kumteua kuwa naibu wa mkurugenzi wa msimamizi masuala ya utenda kazi , wadhifa usiokuwapo katika kaunti ya Kitui.

Jaji Onyango alitoa agizo hilo la kuwazima wawili hao kumwondoa Bw Mutembei katika wadhifa wake mnamo Januari 26 2018.

Jaji Onyango alifahamishwa kuwa mnamo Mei 2 2018 washtakiwa hao wawili (mbiti na kimanzi) walitangaza nafasi ya kazi ya wadhifa aliokuwa akitekeleza.

Bw Mutembei anasema wawili hao walitangaza wadhifa wake kuwa hauna mtu na kualika maombi ya waliotaka kuajiriwa katika wadhifa huo wa Msimamizi wa Utendakazi katika kaunti hiyo ya Kitui.

Wadhifa huo ulitangazwa katika mojawapo ya Magazeti mnamo Mei 5 2018.

Amesema kaunti hiyo ilimwajiri Bw Ngesu kuchukua mahala pake bila idhini ya mahakama.

Pia ameeleza mahakama kuwa wawili hao walikataa kumwagiza aliyekuwa naibu wake Bi Lenah Nduku Moses kumkubalia arudi katika afisi yake baada ya Jaji Onyango kuamuru asiondolewe katika wadhifa wake.

Mnamo Desemba 11 2017 kaunti hiyo ilikuwa imemruhusu Bw Mutembei kuendelea kuhudumu katika afisi hiyo.

Mlalamishi amesema kuwa alikaa muda wa miezi minane bila ofisi ya kufanyia kazi.

Bw Mutembei ameomba mahakama ya ELRC iwasukumue jela miezi isiyopungua miezi sita kwa kukaidi maagizo ya korti.

  • Tags

You can share this post!

Idd-ul-Adha: Usalama waimarishwa Lamu

Benki zakaidi kupunguzia wateja riba ya mikopo

adminleo