• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 9:55 AM
Majonzi washirika 5 wa kanisa moja kuangamia ajalini wakitoka mazishini

Majonzi washirika 5 wa kanisa moja kuangamia ajalini wakitoka mazishini

Na DERICK LUVEGA

KANISA moja katika Kaunti ya Vihiga linaomboleza vifo vya washiriki watano waliofariki kwenye ajali wakitoka mazishini.

Washirika hao wa kanisa la African Divine Church (ADC) walifariki katika ajali mbaya ya barabarani iliyofanyika eneo la Gilgil. Saba kati yao walijeruhiwa.

Washirika watatu wa kanisa hilo, miongoni mwao Kasisi Ernest Aluvale wangali wamelazwa katika hospitali tatu jijini Nairobi wakiwa katika hali mahututi. Wanne kati yao walitibiwa mjini Gilgil na kuruhusiwa kuondoka.

Wakati ‘Taifa Leo’ ilizuru makao makuu ya kanisa hilo katika eneo la Boyani, Vihiga jana, Askofu John Chabuga alikuwa akiongoza kamati inayoandaa mikakati ya mazishi ya kuzikwa kwa watano hao. Askofu Chabuga ndiye kiongozi wa kanisa hilo nchini.

Baada ya mkutano huo, Askofu Chabuga alisema kuwa miili ya watano hao tayari imesafirishwa kutoka Gilgil hadi katika mochari ya Chiromo, jijini Nairobi.

Kutakuwa na ibada ya pamoja Nairobi kabla ya miili hiyo kabla ya mazishi.

Waathiriwa hao ambao wote ni wanawake walitambuliwa kama Beatrice Kavere, Everlyne Avisa, Emily Kageha, Josephine Ataa na Everlyne Karega. Bi Kavere ni mkewe Kaasisi Aluvale ambaye angali hospitalini kutokana na majeraha aliyopata katika ajali hiyo.

Kilomita chache kutoka kanisa hilo kuna familia ya Bi Pamela Chonelwa, ambaye alifariki katika ajali hiyo ila si mshiriki wake.

Nduguye Chonelwa, Aston Emile alitaja kifo cha dadake kuwa pigo kubwa kwa familia hiyo, huku akiwaomba wahisani kujitokeza kuwasaidia.

“Alikuwa mtu mwenye bidii sana, kwani alikuwa akimiliki duka la vyombo vya urembo mjini Mbale,” akasema Emile.

Watu 11 walifariki katika ajali hiyo. Gavana Wilbur Ottichilo ni miongini mwa viongozi ambao wametuma risala za rambirambi.

  • Tags

You can share this post!

Hospitali zinakaribiana na polisi kwa ufisadi – Ripoti

Gavana awarudisha kazini mawaziri kisha kuwapiga kalamu tena

adminleo