Habari Mseto

Mali ya East Africa Cement kupigwa mnada kulipa wafanyakazi

August 15th, 2018 Kusoma ni dakika: 1

Na BERNARDINE MUTANU

Kampuni ya Saruji ya East Africa Cement itapoteza mali yake itakayopigwa mnada kwa lengo la kupata Sh1.4 bilioni ilizodaiwa na wafanyikazi wake.

Hii ni baada ya kampuni hiyo kushindwa kutekeleza makubaliano ya nyongeza ya mshahara (CBA).

Tayari chama cha wafanyikazi katika sekta ya kemikali nchini (KCAWU) imepata huduma za mnadi ambaye ataanza shughuli hiyo punde baada ya kipindi cha notisi kukamilika.

Pesa hizo, Sh Sh1, 401,585,364 zinadaiwa na zaidi ya wafanyikazi 400 katika CBA ya 2013–2015.

Mkataba huo ulizua kesi katika mahakama ya Leba na ile ya Rufaa.