Habari Mseto

Mamia ya mifugo wafa baada ya kunyeshewa

November 1st, 2018 Kusoma ni dakika: 1

Na BERNARDINE MUTANU

Mamia ya mifugo na wanyama wa porini wamefariki kutokana na mvua kubwa iliyonyesha katika Kaunti ya Taita Taveta.

Kulingana na wafugaji, maeneo yaliyoathiriwa zaidi ni mashamba makubwa na maeneo karibu na Mbuga ya Wanyamapori ya tsavo.

Wanyama wadogo wa porini pia hawakusazwa, “Hatujui kinachoua mifugo wetu na wanyama wa porini,” alisema mmoja wa wakazi.

Mashamba ya Kasigau na Amaka na eneo la Kuranza katika mpaka wa Kenya na Uganda yalisemekana kuathirika zaidi kutokana na hali hiyo isiyoeleweka. Zaidi ya mifugo 300 walikufa licha ya kuwa hakuna ugonjwa ulioropitiwa eneo hilo.

Kulingana na wafugaji, mifugo waliokufa walikuwa dhaifu kutokana na ukame na mvua iliponyesha wakafa.

Kaunti hiyo ina mashamba karibu 30 ambayo wakulima hufuga mifugo wakiwemo mbuzi, kondoo, ngamia na ng’ombe.