Maporomoko yazua huzuni Pokot
NA OSCAR KAKAI
Watu wawili walifariki Jumatano usiku baada ya maporomoko kushuhudiwa Weiwei Pokot Magharibi Kaunti ya Pokot.
Maafisa walisema kwamba watu wanne waliokolewa na kupelekwa hospitalini kwa matibabu.
Maporomoko hayo yaliharibu nyumba tano huku watu kadhaa wakipata majeraha.
Chifu wa eneo la Karapogh Benson Seirayai alisema kwamba mvua kubwa iliyoshuhudiwa usiku huo ndiyo ilisababisha maporomoo hayo.
Afisa huyo alisema mwanamke wa niaka 75 na kijana wa miaka sita walizikwa wakiwa hai na mchanga..
Nyumba iliyokuwa na watu wanne ilibebwa na maporomoko hayo lakini kwa bahati nzuri kila mtu aliokolewa.
Bw Seirayai alisema kwamba maeneo yalioathirika hayapitiki kwani juhudi zao za kupeleka miili hiyo Kapenguria hazikufua dafu.
Wakati uo huo chifu huyo pia alisema mifugo kadhaa walizikiwa wakiwa hai na maporomoko..
“Familia tano zimebebwa huwezi jua kwamba kulikuwa na nyumba hapa. Tumepoteza maisha ya watu na mali,” alisema chifu huyo..
Alisema kwamba mwaka jana Novemba maporomoko hayo yalichukua uai wa watu 22 kutoka eneo hilo na wengi wakapata majeraha.
TAFSIRI NA FAUSTINE NGILA