• Nairobi
  • Last Updated March 5th, 2024 1:47 PM
Maraga aagiza korti ya Nanyuki ifungwe

Maraga aagiza korti ya Nanyuki ifungwe

NA FAUSTINE NGILA

Jaji mkuu David Maraga ameagiza kufungwa kwa korti ya Nanyuki kufuatia kuongezeka kwa virusi vya corona.

Jumatano idadi ya maambukizi ya  virusi vya corona kaunti ya Laikipia ilikuwa imefikia 529.

Kupitia kwa hakimu mkuu Hatari Waweru Maraga aliagiza kwamba korti hiyo ifungwe kwa siku 14.

“Jaji mkuu kupitia kwa jaji  wa mahakama kuu Tleo amegiza kufungwa kwa korti ya Nyanyuki kwa siku  14,”alisema Bw Marga Alhamisi.

Kufuatia kufungwa kwa korti hiyo aliagiza kwamba shugli zote zifanyike kwenye mahakama ya Nyeri.

  • Tags

You can share this post!

Polisi wachunguza kisa cha mwenzao aliyejitia kitanzi

Bwanyenye wa Zimbabwe ashangaza alivyopanga maziko yake...