• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 8:55 PM
Mashirika ya serikali yadaiwa Sh1.9 bilioni na NCA

Mashirika ya serikali yadaiwa Sh1.9 bilioni na NCA

Na BERNARDINE MUTANU

MASHIRIKA matatu ya serikali ni miongoni mwa mashirika yanayodaiwa na Mamlaka ya Kitaifa ya Ujenzi (NCA).

Mashirika hayo yanadaiwa jumla ya Sh1.9 bilioni ambazo zililimbikizwa kufikia Januari 2017.

Mashirika hayo ni Mamlaka ya Reli (KRC), Mamlaka ya Barabara za Mashinani (KURA) na kampuni ya Kenya Pipeline Company (KPC).

Mashirika hayo matatu yanadaiwa Sh963.8 milioni (asilimia 54) ya deni lote kufikia mwaka uliokamilika Juni 2017.

Mchunguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Edward Ouko alisema Shirika la Reli lina deni ya Sh625,132,485 kwa NCA, Kura (Sh71,167,350) na KPC (Sh267,542,035).

“Usimamizi wa NCA haukueleza sababu ya mashirika hayo kuwa na deni kubwa kwa muda wa miaka miwili na hatua iliyochukua kupata pesa hizo,” alisema Bw Ouko katika taarifa yake.

Ada ya ujenzi iliondolewa 2016 na serikali kuu kuzisaidia serikali za kaunti na mashirika ya serikali kupunguza gharama ya miradi.

Hii ni baada ya serikali kusema ada hizo zilikuwa kikwazo kwa uwekezaji. Wajenzi ambao miradi yao ilikuwa zaidi ya Sh5 milioni walikuwa wanalipa ada ya asilimia 0.5 kuambatana na thamani ya kandarasi.

  • Tags

You can share this post!

Kesi ya sakata ya NYS yaahirishwa hadi Januari 14

KRA yalenga kukusanya Sh2 bilioni kwa wenye biashara ndogo

adminleo