• Nairobi
  • Last Updated April 28th, 2024 7:50 AM
Matokeo ya upasuaji wa miili ya Bi Kighenda na bintiye yatolewa

Matokeo ya upasuaji wa miili ya Bi Kighenda na bintiye yatolewa

Na CHARLES WASONGA

HATIMAYE miili ya Mariam Kighenda na bintiye Amanda Mutheu ilifanyiwa upasuaji Jumatano, siku nne baada ya kuopolewa kutoka baharini walikotumbukia katika kivuko cha Likoni wakiwa ndani ya gari lao.

Kulingana na mpasuaji mkuu wa serikali Johansen Oduor, shughuli hiyo ambayo iliendeshwa kwa muda wa saa moja na nusu ilibainisha kuwa wawili hao walifariki baada ya kukosa uwezo wa kupumua.

Upasuaji huo ulifanyika katika hifadhi ya maiti ya Hospitali ya Jocham mjini Mombasa ambako miili imehifadhiwa.

Kwenye taarifa kwa wanahabari, msemaji wa familia ya marehemu Luka Mbati ameelezea kuridhishwa na matokeo ya upasuaji wa miili hiyo akisema mipango ya mazishi sasa itaanza.

“Kama familia tumetosheka na matokeo ya upasuaji kama yalivyotangazwa na Dkt Johansen Oduor. Sasa tunaanza mipango ya mazishi,” akasema Bw Mbati.

Mazishi yatafanyika nyumbani kwa mumewe Bi Kighenda, John Wambua, katika Kaunti ya Makueni.

Marehemu Kighenda na bintiye walikufa maji mnamo Septemba 29, 2019, gari lao lilipoteleza kutoka kwa feri ya MV Harambee na kutumbukia katika Bahari Hindi.

Gari hilo liliopolewa baada ya siku 13 katika operesheni iliyoendeshwa na wapigambizi kutoka asasi mbalimbali za humu nchini na wakisaidiana na wale waliitwa kutoka nchini Afrika Kusini.

  • Tags

You can share this post!

Magavana hawakuhusishwa katika mradi wa ukodishaji wa vifaa...

Aukot adai Mswada wa Punguza Mizigo uliyumbishwa na...

adminleo