Mawakili wataka korti zifunguliwe mrundiko wa kesi upungue
Chama cha Mawakili tawi la Mombasa kimesema kuwa katiba haiwezi kutekelezwa katika hali ambayo korti zimefungwa.
Mwenyekiti wa chama hicho Mathew Nyabena alisema kuwa Jaji Mkuu anapaswa kubadilisha uamuzi wake na kuruhusu shughuli za kawaida kuendelea kila siku kwa kufuatilia hali ya janga la corona.
“Tunawaomba baadhi ya mahakimu wawe wakishughulikia maswala ya kila siku,” alisema Bw Nyabena, akiongezea kuwa kunapaswa kuwa na wafanyakazi wachache katika afisi za usajili kushungulikia kukusanya stakabathi za mawakili na washtakiwa.
Bw Nyabena aliogezea kuwa kuna kesi za dharura ambazo zinapaswa kusikizwa kwa wakati unaofaa.
Alisema kuwa Jaji Mkuu amezuia majaji na wakuu wa vituo kubuni mbinu mbadala za kufanya kazi,
Bw Nyabena alisema kuwa imekuwa kazi ngumu kwa mawakili kutekeleza majukumu yao kutokana na notisi iliyotolewa kuwa ni kesi za dharura pekee zitakazosikizwa kila Alhamisi pekee.