• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 6:39 PM
Mazishi ya Mbunge yapigwa breki

Mazishi ya Mbunge yapigwa breki

Na RICHARD MUNGUTI

MAZISHI ya aliyekuwa Mbunge wa Matungu, Justus Murunga Makokha yamesimamishwa hadi kesi iliyowasilishwa na mwanamke anayedai kuwa mke wake wa tatu isikilizwe na kuamuliwa.

Na wakati huo huo, chumba cha kuhifadhia maiti cha Lee Funeral kimeagizwa na Mahakama ya Milimani kisiachilie mwili wa Murunga hadi kesi iliyowasilishwa na Agnes Wangui Wambiri isikizwe na kuamuliwa.

Akitoa agizo hilo, hakimu mkazi Bi A N Makau pia aliamuru sampuli za DNA zitolewe katika mwili wa Murunga zipimwe kubaini ikiwa ndiye baba wa watoto wawili ambao Wangui adai alizaa naye.

Bi Makau aliagiza kesi hiyo isikziwe Novemba 26, 2020. Mahakama ilisema kuwa, kesi ya Wangui iko na mashiko kisheria kwa vile inahusisha masuala ya watoto.

“Masuala na haki za watoto hayakomi mzazi anapoaga,” wakili Danstan Omari anayemwakilisha wakili wa mlalamishi alisema.

Bi Wangui aliomba mahakama iamuru aruhusiwe kushiriki mipango ya mazishi ya marehemu.

“Mlalamishi pamoja na watoto wake wanataka wahusishwe katika mipango ya mazishi ya Murunga,” alisema Omari.

Hakimu huyo alimwamuru Bw Omari awakabidhi nakala za kesi wake wawili wa marehemu pamoja na wasimamizi wa mochari ya Lee Funeral jijini Nairobi.

“Baada ya kusoma ushahidi uliowasilishwa na kusikiza pande zote, nimefikia uamuzi kwamba kesi ya Wangui iko na mashiko kisheria kwa vile haki za watoto wawili zinaweza kukandamizwa iwapo hawataruhusiwa kushiriki mazishi ya baba yao,” alisema Bi Makau.

  • Tags

You can share this post!

DOMO KAYA: Nai-Fest inazidi kukosa shangwe

Hofu vifo kutokana na Covid-19 vikiendelea kuthibitishwa