• Nairobi
  • Last Updated April 28th, 2024 4:55 PM
Mbunge akamatwa kwa kuchochea maandamano

Mbunge akamatwa kwa kuchochea maandamano

NA ERIC MATARA

Mbunge wa Nakuru Mashariki David Gikaria amekamatwa kuhusiana na maandamnao yaliyoshuhudiwa Jumatatu asubuhi.

Kamanda wa polisi wa kaunti hiyo Tito Kilonzi alisema mbunge huyo alichochea maandamano hayo yaliyoathiri shughuli za biashara katikati mwa mji wa Nakuru.

“Mbunge huyo amekamatwa na kuzuiliwa kwenye kituo cha polisi cha Nakuru ya kati. Mbunge huyo pamoja na watu wengine ambao maafisa wangu wanatafuta walichochea maandamano yaliyoshuhudiwa kwenye mji wa Nakuru,” alisema Bw Kilonzi.

Bw Gikaria alikamatwa baada ya kufika kwenye afisi za kaunti akidai kwamba alihongwa ili apeane maafisa wa polisi watulize waandamanaji. Bw Kilonzi alisema kwamba mbunge huyo alikamatwa afisini kwake.

Bw  Gikaria aliachiliwa baadaye kwa dhamana yaa Sh10,000 ambayo ililipwa na mwezake wa eneo bunge ya Nakuru Magharibi Samuel Arama. “Aliangizwa kuripoti tena kwenye kituo cha polisi Ijumaa alisema,” Bw Kilonzi.

Mji wa Nakuru uligeuka kuwa wa vita huku watu wa matatu na wanapolisi wakikimbizana kufuatia maamuzi ya gavana wa kaunti hiyo Lee Kinyanjui ya kufunga mji wa Nakuru magari ya abiria yasiingie.

Wafanyakazi hao wa matatu walilaumu kaunti hiyo kwa kukosa kuwashirikisha kabla ya kutekeleza hayo.

Sehemu nyingi za mji wa Nakuru ziligeuka kuwa za vita huku polisi wakikabiliana na wananchi.

TAFSIRI NA FAUSTINE NGILA

  • Tags

You can share this post!

Hasara maziwa mawili yakizamisha ardhi

Wapenzi wasema walimuua mtoto kuokoa uhusiano wao