• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 11:53 AM
Mgomo wa madaktari Nakuru wasitishwa

Mgomo wa madaktari Nakuru wasitishwa

Joseph Openda

Mgomo wa madakatari wa kaunti ya Nakuru uliokuwa uanze Jumatatu umesitishwa kwa muda.

Hii ni baada ya muungano wa KMPDU kutia sahihi mkataba na serikali ya kaunti hiyo na kusimamisha  mgomo huo ambao notisi yake ilitolewa Agosti 11.

Mwenyekiti wa KMPDU Davji Atellah alisema kwamba muungano huo ulikubali kusitisha mgomo huo ili kuruhusu kutekelezwa kwa makubaliano yao.

Dkt Atellah akihutubia wanahabari alisema kwamba serikali ya kaunti ilikubali kutekeleza mahitaji yao na walikuwa tayari kujadiliana kuhusu suala lililobaki.

“Notisi ya mgomo ya siku 21 ilikuwa imalizike leo lakini baada ya mazungumzo na serikali ya kaunti tumefikia uamuzi kwamba tusiendelee na mgomo,”alisema Dkt  Atella.

Serikali ya kaunti pia ilihaidi kuajiri madakatari zaidi kati ya muda wa miaka tano ili kutimiza mahitaji ya madaktari na kuwapa madaktari mkopo wa magari wa malipo ya polepole.

Mmoja wa kamati ya kuhungulikia maswala ya afya ya kaunti hiyo Dkt Gichuki Kariuki alisema kwamba maswala ambapo madaktari wamekuwa wakitaka yashungulikiwe hayajaishungulikiwa kwa miaka Zaidi ya kumi..

“Serikali ya Kaunti ya Nakuru ni waajiri wanaoelewa wajibu wao na pia wanaelewa maana ya wafanyakazi wa afya hasawakati huu wa janga la corona. Tayari tumeanza kuweka mikakati kuhakikisha kwamba maswala ya maafisa wa afya  yameshughulikiwa,”alisema Dkt Kariuki.

Tafsiri Na Faustine Ngila

  • Tags

You can share this post!

Obure na Ouko kushtakiwa kwa mauaji

Hofu jijini magenge yakipora watu mchana