• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 3:09 PM
Miili yazidi kupatikana mitoni jiji la Nairobi likisafishwa

Miili yazidi kupatikana mitoni jiji la Nairobi likisafishwa

Na Sylvania Ambani

SHUGHULI ya kusafisha jiji la Nairobi inayoendelezwa na utawala wa Gavana Mike Sonko, imepelekea kupatikana miili minne kufikia sasa ndani ya mito na inahofiwa huenda idadi ikaongezeka.

Jumamosi, mwili wa mwanamume mwenye umri wa makamu ulipatikana katika Mto Ngong karibu na Wadi ya Kware, eneo la Embakasi Kusini.

Vijana walioajiriwa chini ya mpango wa ‘Ng’arisha Jiji’ walipata mwili huo ambao ni wa nne kupatikana tangu Bw Sonko alipoanzisha shughuli hiyo mwaka uliopita.

Miili yote minne imekuwa ikipatikana katika Mto Ngong japo maeneo tofauti ya mto huo.

“Hizi ni baadhi ya changamoto ambazo wahudumu wamekuwa wakipitia wanaposafisha mito ya Nairobi. Nimeita polisi wa eneo hilo na wanasaidia kuondoa mwili mtoni,” akasema gavana huyo.

Mpango wa ‘Ng’arisha Jiji’ ulizinduliwa na mkewe gavana, Bi Primrose Mbuvi ili kusafisha jiji hilo ambalo limekuwa likikumbwa na tatizo la uzoaji taka. Kazi ya vijana wanaohusika huwa ni kuondoa taka mitaani kwa jumla.

 

  • Tags

You can share this post!

Polisi wavunja kambi ya MRC msituni na kunasa silaha

Wanafunzi 2 wafa shuleni katika hali tatanishi

adminleo