Habari Mseto

Miradi yakwama kutokana na utovu wa usalama

June 7th, 2020 Kusoma ni dakika: 1

By BARNABAS BII

Miradi ya mamilioni ya pesa ya unyunyiziaji maji inayolenga kuongeza uzalishaji wa chakula katika maeneo kame magharibi ya nchi ina uwezekano wa kusambaratika kwa sababu ya migogoro ya mipaka na wizi wa mifugo.

Miradi hiyo ya kaunti za Pokot Magharibi, Turkana, Samburu na Elgero Marakwet imekuwa ikipata pigo kubwa kwa sababau ya vita dhidi ya jamii za wafugaji huku vilivyoweka maisha ya familia 4,500 wanaotengea miradi hiyo kwa chakula mashakani.

Kamishna wa polisi wa Bonde la Ufa aliwaomba wakazi wasalimishe silaha walizo nazo kinyume na sheria na kushirikiana na maafisa wa usalama ili kupigana na uhalifu.

Afisa huyo hivi karibuni aliandaa mkutano Eldoret na maafisa wakuu wa usalama kutoka Turkana, Baringo, Pokot Magharibi, Elgeyo Marakwet na kaunti ya Laikipia ambapo alisema kwamba kuongezeka kwa silaha kinyume na sheria miongoni mwa wafugaji kumezorotesha usalama na maendeleo eneo hilo.

Mwaka huu mambo yamekuwa magumu kwa sababu ya mafuriko yalioharibu miradi mingi ya maendelo Kerio Valley.