• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 7:50 PM
Misa ya ukumbusho wa Jenerali Ogolla yaahirishwa

Misa ya ukumbusho wa Jenerali Ogolla yaahirishwa

VICTOR RABALLA NA LABAAN SHABAAN

IDARA ya Jeshi Kenya (KDF) imeahirisha misa ya ukumbusho wa marehemu Jenerali Ogolla iliyoratibiwa kufanyika Ijumaa Aprili 26.

Haya ni kwa mujibu wa tangazo la pamoja la KDF na familia ya Jenerali Ogolla.

“Tarehe mpya ya hafla ya ukumbusho itakayofanyika katika uga wa michezo ya Ulinzi itatangazwa baadaye,” ilisema taarifa hiyo.

 “Hata kama siku tatu za maombolezi ya kitaifa zilikamilika na tunaendelea tena na maisha bila Jenerali Ogolla, pamoja tunaendelea kuombea familia na wenzetu walioangamia katika ajali ya helikopta,” taarifa ilieleza zaidi.

Ibada ya Ijumaa ilikuwa imepangwa kuendana na matakwa ya familia.

Walishukuru wote waliotuma risala za rambirambi na kuomboleza nao baada ya wanajeshi 10 kuaga dunia katika ajali ya ndege Alhamisi Aprili 18.

Vile vile, walimshukuru Rais William Ruto kwa kuongoza taifa katika ibada ya heshima za kijeshi Nairobi na ile ya mazishi ya kitaifa kijijini Ng’iya, Kaunti ya Siaya.

Idara ya jeshi na familia ya Jenerali Ogolla kadhalika iliwashukuru Mama wa Taifa Rachel Ruto, Bi Dorcas Rigathi pamoja na serikali za kaunti na ya kitaifa.

Ndege ya kijeshi ilianguka juma lililopita eneo la Sindar, Kaunti ya Elgeyo Marakwet wakati maafisa wa jeshi walisafiri kukagua shule na kuimarisha usalama maeneo ya Bonde la Ufa.

Maafisa wawili wa jeshi walinusurika na wanaendelea kupokea matibabu hospitalini.

  • Tags

You can share this post!

Murkomen: Afisi yangu haihusiki na uchunguzi wa ndege...

Mkurugenzi kizimbani kwa kughushi wosia wa marehemu

T L