• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 11:42 PM
Mjukuu wa bilionea Karume afa baada ya kukosa hela za tiba

Mjukuu wa bilionea Karume afa baada ya kukosa hela za tiba

Na WANJOHI GITHAE

MOJAWAPO ya wajukuu wa mwanasiasa Njenga Karume, aliyefariki mnamo Jumamosi nchini Amerika, alikuwa ameomba fedha za kugharimia matibabu yakena kukosa kutumiwa, Taifa Leo imebaini.

Bi Michelle Wariara Karume, 25, alifariki mjini Houston, jimboni Texas, baada ya kuugua saratani kwa muda mrefu.

Mnamo Machi 21, mwaka huu, aliandika barua pepe yenye hisia, akiwaomba wasimamizi wa mali ya Bw Karume kumsaidia kifedha.

Bi Wariara ni mwanawe marehemu Joseph Karume Njenga, aliyekuwa mwanawe Bw Karume.

Bi Wariara amekuwa akiugua ugonjwa huo tangu mwaka 2014.

Duru kutoka kwa familia hiyo zilisema kuwa fedha hizo zilitolewa mnamo Mei, lakini wakati huo ulionekana kuchelewa, kwani ugonjwa ulikuwa umemwathiri vibaya.

Barua pepe hiyo ilitumiwa Bw George Waireri, ambaye ni mmoja wa wasimamizi wa mali hiyo pamoja na jamaa zake.

Lakini jana, Bw Waireri alisema kuwa kifo cha marehemu hakihusiani na ukosefu wa fedha.

“Alikuwa nchini Amerika kwa zaidi ya mwaka mmoja akipokea matibabu. Hakihusiani kwa vyovyote na ukosefu wa fedha. Kifo hicho kilitokana maradhi ya saratani. Alipata usaidizi aliohitaji lakini maumivu yakamzidi,” akasema.

Hata hivyo, kauli yake ilipingwa vikali na wakili wa watoto wa Bw Karume, Bw Peter Munge, aliyesisitiza kuwa Bi Wariara alifariki kwa kukosa fedha za matibabu.

“Mara kadhaa, tulilazimika kwenda mahakamani ili kushinikiza apewe fedha za kugharamia matibabu yake. Kwa wakati mmoja, marehemu alibubujikwa na machozi mahakamani, akiwaomba wasimamizi wa mali hiyo kumpa fedha za matibabu,” akasema.

  • Tags

You can share this post!

Mabwawa: Hatua ya Rais yachemsha ngome ya Ruto

Wakenya wanapenda minofu ya kuku kuliko nyama ya...

adminleo