• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 8:55 AM
MKU yafadhili ujenzi wa darasa nchini Rwanda

MKU yafadhili ujenzi wa darasa nchini Rwanda

Na LAWRENCE ONGARO

CHUO Kikuu cha Mount Kenya (MKU) kimejitolea kujenga darasa moja katika shule mojawapo ya msingi nchini Rwanda.

Mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya GroupScolaire de Gahanga, Bw Felix Niyitegeka, alikipongeza chuo cha MKU kwa kujitolea mhanga kuona ya kwamba  wanafunzi wa shule hiyo wanapata mafunzo katika mazingira mema.

“Ninamshukuru sana mwanzilishi wa Chuo hicho Prof Simon Gicharu kwa kazi nzuri ambayo ametufanyia ya kutujengea angalau darasa la wanafunzi wa shule ya msingi,” alisema Bw Niyitegeka.

Profesa Simon Gicharu akikabidhi hundi ya fedha kwa wasimamizi wa shule ya msingi ya Group Scolaire de Gahanga ya Rwanda. Picha/ Hisani

Darasa hilo ambalo ni la kisasa litaweza kuhimili wanafunzi wapatao 46, huku ikitarajiwa umeme utasambazwa hapo, tangi la maji litawekwa na pia litakuwa na madawati ya kisasa kabisa, alifafanua mwalimu huyo.

“Kwa sasa ujenzi wa shule hiyo unaendelea ambapo wanafunzi watakaorejea muhula wa pili watapata nafasi nzuri ya kuingia kwa darasa hilo litakalokuwa na vifaa vyote muhimu,” alisema.

Alisema ushirikiano wao na MKU umezaa matunda na wanamshukuru sana Prof Gicharu kwa kazi yake nzuri.

“Mara ya kwanza tulipokutana naye alisema alikuwa tayari kuona ya kwamba Chuo Kikuu cha Mount Kenya kinafanya jambo la kusaidia wanafuzi na ndiyo maana aliamua kujenga darasa kwa wanafunzi,” alisema Bw Niyitegeka.

Alisema shule hiyo ya msingi bado inahitaji ufadhili zaidi kwa sababu wanafunzi ni wengi na kuna msongamano mkubwa katika shule hiyo.

Kulingana na mwalimu huyo darasa hilo lilizinduliwa mnamo Februari 2019 na litakamilika vizuri ifikapo mwezi Mei jinsi ilivyopangwa.

Alisema iwapo shule hiyo itazidi kupokea ufadhili zaidi na bila shaka itapata mwamko mpya na hata wanafunzi watapata motisha zaidi kujiendeleza kielimu.

Kuboresha

Naibu Chansela wa kitengo cha MKU nchini Rwanda, Profesa Edwin Odhuno alisema ushirikiano wa chuo hicho na shule hiyo ya msingi utaboreshwa zaidi katika siku zijazo.

“Tutafanya juhudi kuona ya kwamba tunashirikiana na washikadau wote ili tuweze kuinua maisha ya wakazi wa Rwanda kwa njia moja au nyingine. Pia tuko tayari kuzuru maeneo kadha ili kuelewa jinsi wanavyoendesha mambo yao hasa ya kimaendeleo,” alisema Prof Odhuno.

  • Tags

You can share this post!

MAPISHI: Sambusa za mboga

WAKILISHA: Mtetezi wa mabinti dhidi ya ukeketaji

adminleo