Mmiliki wa basi lililoua watu 55 ndani
Na CHARLES WASONGA
POLISI Jumatano jioni Jumatano jioni walimkamata mmiliki wa basi ambalo lilisababisha ajali na kusababisha vifo vya watu 55 siku hiyo Alfajiri katika eneo la Fort Tenan katika barabara ya Londiani- Muhoroni
Kamanda wa trafiki kaunti ya Kakamega Willy Kamuren alisema Bw Bernard Ishindu Shitiabayu alikamatwa mjini Kakamega. Mwingine aliyekamatwa na mwanachama wa kampuni ya Western Cross Express Sacco Bw Cleophas Shimanyula. Basi hilo linasimamiwa na kampuni hiyo.
Wawili hao wanazuiliwa katika Kituo cha Polisi chja Kakamega Central ambako wanahojiwa huku uchunguzi ukiendelea kubaini chanzo cha ajali hiyo.
Inspekta Jenerali wa Polisi Joseph Boinnet alisema mmiliki wa basi hilo atashtakiwa kortini kwa sababu haikuwa na leseni ya kuhudumu nyakati za usiku.
Mamalaka ya Usalama Barabarani (NTSA) ilithibitisha kuwa basi hilo lenye nambari ya usajili ya KBJ 029J, haipatikani katika tovuti yake.
Japo Mkurugenzi Mkuu wa NTSA Francis Meja alisema basi hilo halikuwa na leseni, duru zilisema kuwa huwa linahudumu katika ruti ya Nairobi – Magharibi mwa Kenya nyakati za usiku.