• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 8:55 PM
Monda apata pigo lingine kortini katika juhudi za kukwamilia unaibu gavana

Monda apata pigo lingine kortini katika juhudi za kukwamilia unaibu gavana

NA RUTH MBULA

NAIBU Gavana wa Kaunti ya Kisii aliyefurushwa, Dkt Robert Monda, amepata pigo lingine baada ya Mahakama Kuu ya Nyamira kuruhusu kuondolewa kwa mojawapo ya kesi alizowasilisha kujitetea.

Japo mlalamishi, Bw Jared Mairura Ratemo, alikuwa binafsi amewasilisha ombi la kuondoa kesi hiyo, Jaji Wilfrida Okwany alichukulia hatua hiyo kuwa yenye nia mbaya akiitaja kama “ujanja” unaolenga “kutumia vibaya mchakato wa korti.”

Mawakili Katwa Kigen na Wilkins Ochoki, waliomwakilisha “mhusika aliyekusudiwa” (Dkt Monda) walimsihi Jaji Okwany asiruhusu kesi hiyo kuondolewa.

Wawili hao walihoji kuwa hatua ya kuondoa kesi hiyo inakiuka kanuni na kwamba kesi hiyo inahusu maslahi ya umma yanayopaswa kupatiwa uzito zaidi ya hatua ya awali ya mlalamishi.

Jaji Ochieng Oginga, akimwakilisha “mshtakiwa aliyekusudiwa” aliunga mkono hatua hiyo ya kuondoa kesi, akitaja kukiukwa kwa kanuni za mahakama kwa misingi kuwa hatua ya mlalamishi kuondoa kesi inaashiria mwisho wa kesi kwa sababu inamaanisha kujiondoa na malalamishi yote.

Bw Ratemo alikuwa mwanzo amewasilisha kesi mbele ya Mahakama Kuu ya Machakos ambapo alipata kibali cha muda cha kuendelea na hali ilivyokuwa kuhusu kushikilia afisi ya Naibu Gavana Kaunti ya Kisii.

Jaji Francis Rayola alisema mlalamishi alizua maswali nyeti kuhusu mchakato huo kikatiba.

  • Tags

You can share this post!

Mahakama yaagiza Sh13.4m za Mathe wa Ngara ziendee serikali

Hana haraka ya kunioa rasmi japo aliahidi nikishajifungua

T L