• Nairobi
  • Last Updated May 7th, 2024 9:48 PM
Moto walamba bweni nzima Shule ya Upili ya Musingu

Moto walamba bweni nzima Shule ya Upili ya Musingu

NA BENSON AMADALA

Moto ulizuka Jumatano na kuchoma bweni moja katika Shule ya Upili ya Musingu Kaunti ya Kakamega siku mbili baada ya wanafunzi kurudi shuleni.

Kamanda wa polisi wa kaunti ndogo ya Kakamega Joseph Chesire alisema wakazi walijaribu kuzima moto huo lakini wakalemewa.

Moto huo ulianza saa tano na nusu asubuhi wakati wanafunzi walikuwa darasani. Wanafunzi waliangalia moto ukiteketeza vitu vyao huku wakikosa la kufanya.

Bweni ambalo wanafunzi 100 hulala kimeteketea lakini hakuna mtu aliyeumia. Bweni lenye vitanda 500 pia liliteketea.

Kilichosababisha moto huyo hakijulikani. Chumba ambacho kilijengwa na serikali ya kaunti yya Kakamega na kuitwwa jina la gavana Wycliffe Oparanya ambaye alisomea shule hiyo kilisemekana kuwaka moto wakati mafundi wa vyuma walikuwa wanatengeneza dirisha zilizokuwa zimevunjika.

Shule hiyo ina mabweni manne na lile la Oparanya linaweza kulala wanafunzi 504.

Wanafunzi wa kidato cha nne 266 walikuwa tayari washarudi shule wakati moto huo ulizuka. Hii ni tukio la tatu la moto kuchoma shule hiyo chini ya miaka miwili.

Tukio kama hilo lilishuhudiwwa Novemba 2019 wakati wanafunzi wa kidato cha nne walipokuwa wakifanya mtihani.

TAFSIRI NA FAUSTINE NGILA

  • Tags

You can share this post!

Amuua nduguye mkubwa kwenye wakizozana

Ruto awaondolea lawama polisi waliovuruga mikutano yake