• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 9:50 AM
Nairobi yapitisha mswada wa kuunda mtandao wa kijamii kutangaza biashara za juakali

Nairobi yapitisha mswada wa kuunda mtandao wa kijamii kutangaza biashara za juakali

NA WINNIE ONYANDO

BUNGE la Kaunti ya Nairobi limepitisha mswada wa kuunda mtandao wa kijamii utakaowawezesha wafanyabiashara wadogowadogo wa sekta ya juakali kutangaza huduma zao kwa wateja, hatua inayoaminiwa itawafungulia fursa nzuri za mapato.

Mswada huo uliwasilishwa na diwani wa Clay City Mwaura Samora.

Kulingana na Bw Samora, wafanyabiashara hao watapata fursa kujiendeleza kibiashara na hata kuchangia mapato ya kaunti kupitia mtandao huo wa kijamii.

“Hii itawawezesha kupata nafasi za ajira. Mtandao huo wa kijamii utakuwa kama majukwaa ya Uber na Bolt. Ukishajisajili, unaunganishwa na mteja na ukifanya kazi bora, hivyo unakuwa na uwezo wa kupata wateja zaidi,” akasema Bw Samora.

  • Tags

You can share this post!

Jifunze namna ya kutumia jiwe la kusaga unga kitamaduni

Raila apigwa jeki na Azimio, Serikali AUC

T L