• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 6:39 PM
Mtoto wa marehemu Sharon kuzikwa Alhamisi

Mtoto wa marehemu Sharon kuzikwa Alhamisi

Na RUTH MBULA

FAMILIA ya mwanafunzi Sharon Otieno aliyeuawa kikatili, imesema kuwa itamzika mtoto wake ambaye hakuwa amezaliwa Alhamisi, huku wakimwomba Rais Uhuru Kenyatta kuhakikisha mwana wao amepata haki.

Jana, familia hiyo ilisema kuwa imeshangazwa na kiwango cha ukatili ambao ulipelekea hata kifo cha mtoto ambaye hakuwa amezaliwa. Walieleza kuwa hadi sasa, hawajaelewa sababu ya mauaji ya Sharon na mtoto wake.

Familia hiyo ilionekana yenye mawazo na maswali mengi kuhusu makosa ambayo marehemu alifanya, kiasi cha kuuawa kikatili. Sura zao pia zilionekana kusawijika, wasijue

“Ni hali ngumu sana kwetu. Mbona wakamuwa kikatili namna hiyo? Ninataka kujua sababu ya mwanangu kuuawa,” akasema Bi Melida Auma, mamake marehemu.

Mwanafunzi huyo wa miaka 25 alikuwa akisomea taaluma ya uwekaji rekodi za matibabu.

“Ni ombi langu kwa Rais Kenyatta kuhakikisha kuwa amefuatilia suala hili ili kuhakikisha ukweli kamili unabainika,” akasema Bi Auma.

Alisema kuwa kifo hicho kimemwathiri sana, ikizingatiwa kuwa Sharon ndiye alikuwa mtoto wake wa kwanza. Alisema kuwa anahitaji maombi ili kurejea katika hali yake ya kawaida.

“Tumepitia hali ngumu sana tangu Sharon alipotoweka. Tunataka suala hili kukamilishwa kwa haraka. Tunataka amani, ila hili litawezekana baada ya wauaji wake kupatikana na kufikishwa mahakamani,” akasema Bi Auma, ambaye ana watoto wanne.

Alieleza kuhusu matumaini makubwa aliyokuwa nayo kwa mwanawe ambayo yalikatizwa ghafla na kifo hicho.

Wapelelezi bado wanaendelea na uchunguzi kuhusu mauaji hayo ambayo yameshtumiwa na wengi kote nchini.

You can share this post!

USHURU: Uhuru alivyotegwa

Mama akiri kumuuza mtoto wake kwa Sh1,200

adminleo