• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 8:57 PM
Mume hajagusa tunda kwa miaka miwili, kila siku alaumu uchovu kazini

Mume hajagusa tunda kwa miaka miwili, kila siku alaumu uchovu kazini

SHANGAZI,

Mpenzi wangu ni mwanamume wa miaka 52. Anafanya kazi lakini mapato yake ni duni. Nimekuwa nikimpa pesa aboreshe maisha yake. Chumbani pia nampakulia vizuri. Sasa nimegundua anatembea na wasichana wachanga. Ni kwa nini?

Ingawa hujafichua umri wako, inawezekana tabia ya mpenzi wako imechochewa na tofauti ya umri kati yenu ndiposa ananyemelea wanawake wachanga. Ni muhimu ujue mpango wake ili usiendelee kupoteza pesa na wakati wako.

Mume hajachovya kwa mzinga miaka 2 sasa!

Nina miaka 38, nimeolewa na nina watoto wawili. Mume wangu amesusia wajibu wake chumbani kwa miaka miwili sasa. Alianza kwa madai ya kuchoka kutokana na kazi hadi sasa imekuwa kawaida. Ninaumia, nishauri.

Hiyo ni hali ngumu kwa mwanamke mchanga kama wewe. Huo ni wajibu muhimu kwa mume na mke. Huenda mume wako hana hisia kwako ama amechoka na ndoa na anashindwa kukwambia. Muhimu mshauriane kwa uwazi ili mjue mwelekeo wa ndoa yenu.

Mke wa bosi anasinya, eti hataki nivae nipendavyo

Nimeajiriwa katika kampuni ya mtu na mkewe na mume ndiye bosi wangu. Mkewe analalamika kuhusu mavazi yangu na ametishia kunifuta kazi nisipobadilisha. Nifanye nini?

Elewa mke wa bosi yuko hapo kulinda biashara na pia familia. Anafikiri mavazi yako yanalenga kunasa mumewe hata iwapo huna nia hiyo. Itabidi ufuate maagizo yake ili uhifadhi kazi yako.

Nimepata demu ila kuna ripoti zimenichanganya

Nimevutiwa kimapenzi na mwanamke tunayefanya kazi pamoja. Ninaamini yeye pia ananipenda. Lakini rafikiye amenionya alikuwa na wanaume wengi awali. Nimechanganyikiwa.

Ni kawaida ya mtu kuwa na wapenzi kadhaa kabla hajapata mwenzake wa maisha. Ninaamini mwanamke huyo amekuwa na wanaume wengine akitafuta mpenzi wa dhati na pengine hajampata. Fuata moyo wako.

  • Tags

You can share this post!

Wataalamu Nyandarua wahimizwa kurejea nyumbani ili...

Viongozi wapamba mikutano ya basari kwa burudani wakiishia...

T L