Mume mpenzi ananipa raha mara moja kwa wiki, miye nataka mara 3
SHANGAZI,
Mwanamume mpenzi wangu amekuwa akitenga muda wa kunipa raha mara moja kila wiki. Nampenda sana na namhitaji angalau mara tatu. Lakini naogopa kumwambia asije akanielewa vibaya. Naomba ushauri.
Mapenzi hufanya watu kuwa kitu kimoja na kuwa huru kushauriana kuhusu jambo lolote lile. Haitakuwa makosa kwako kumwelezea mpenzi hisia zako ambazo zinatokana na mapenzi yako kwake. Kama anakupenda ataelewa.
Demu amesisitiza hataki mtoto hata mmoja
Nimeamua kumuoa mchumba wangu wa miaka mitatu. Amekubali ombi langu lakini amenipa sharti moja. Anataka tuishi sisi wawili tu, hataki mtoto hata mmoja katika maisha yake.
Watu wengi hufunga ndoa ili kuendeleza kizazi kwa kupata watoto. Lakini pia inategemea maelewano ya wahusika. Mchumba wako amekupa sharti ili awe mke wako. Kama shabaha yako ya ndoa ni watoto, itabidi umuache utafute mwingine.
Niko 35, singo na sitaki mtu; kuna shida?
Nina miaka 35 na sina mpenzi. Sababu ni kuwa siamini kuna mapenzi ya dhati. Nimeamua sitawahi kuwa na mpenzi wala mume. Mapenzi yangu ni ya pesa. Kuna shida?
Huo ni msimamo wako binafsi kuhusu mapenzi na ndoa. Kuna wengine wasiokubaliana nawe kwa sababu wanaamini kuna mapenzi ya dhati. Ni haki yako kuishi maisha unayotaka.
Mke wa rafiki yangu alia jamaa amesusia huba
Juzi mke wa rafiki yangu alinipigia simu akitaka kuniona. Tulipokutana aliniambia mumewe amesusia majukumu yote nyumbani. Amesusia pia wajibu ya chumbani. Sasa anataka nizungumze naye.
Mke wa rafiki yako anataka kukutumbukiza ndani ya moto. Hata kama wewe ni rafiki wa familia, hayo ni mambo ya kibinafsi usiyofaa kuingilia. Utamwambia ulikuwa unafanya nini na mkewe ndipo akakwambia hayo? Usikubali.