• Nairobi
  • Last Updated April 28th, 2024 6:50 AM
Mume na mke kizimbani kwa kuibia Chase Bank mamilioni

Mume na mke kizimbani kwa kuibia Chase Bank mamilioni

Na RICHARD MUNGUTI

MTU na mkewe walishtakiwa Jumatano kuibia benki iliyowekwa chini ya mrasimu ya Chase Bank zaidi ya Sh58 milioni.

Bw Mohammed Nasrufullah Khan na mkewe Amira Claudia Wagner Khan walishtakiwa mbele ya hakimu mwandamizi Bi Martha Mutuku katika Mahakama ya Milimani Nairobi.

Wawili hawa wameshtakiwa pamoja na wakurugenzi wakuu wa Benki wanaokabiliwa na shtaka la kuibia benki hiyo inayosimamiwa sasa na Kenya Commercial Bank (KCB) walioshtakiwa mwaka uliopita.

Walioshtakiwa awali mbele ya Bi Mutuku ni washukiwa kumi ambao ni aliyekuwa mwenyekiti wa benki hiyo na nduguye Nasrufullah , Bw Mohammed Zafrullah Khan , aliyekuwa mkurugenzi wa benki hiyo Bw Duncan Kabui Gichu, aliyekuwa meneja mkuu Bw James Mwaura Mwenja, msimamizi wa masuala ya fedha Bw  Makarios Omondi Agumbi , makampuni ya Cammella Investments Ltd, Colnbrook Holdings Ltd, Golden Azure Investments Limited na Cleopatra Holdings Ltd.

Washtakiwa wote kumi wanaotetewa na wakili Cecil Miller walikanusha shtaka la kufanya njama za kuilaghai benki hiyo Sh529,328,000 na Dola  za kimarekani ($) 1,326,000 (sawa na Sh132,600,000) .

Shtaka lilisema walifanya njama hizo kati ya Agosti 28, 2009 na Machi 3 2016 katika afisi za benki hiyo mjini Nairobi.

Upande wa mashtaka ulisema washtakiwa walihamisha mamilioni hayo kwa akaunti za  makampuni haya ya  Cleopatra,Golden na Colnbrook wakidai zilikuwa za mikopo waliyoomba benki hiyo.

Mabw Zafrullah, Gichu. Mwenja . Agumbi  na Camella Holdings Limited walikana waliiba Sh483,328,000 mali ya benki hiyo ya Chase Bank mnamo Desemba 31 2015

Mabw Zafrullah , Gichu na Camella walikana waliiba Sh483,328,000 mnamo Desemba 31 2015 kutokana na nyadhifa zao kama wakurugenzi wa benki hiyo.

Mnamo Feburuari 28 2012 Mabw Zafrullah , Gichu , Mwenja, Agumba na Colnbrook walidaiwa waliiba Sh46milioni.

Mabw Mwenja na Agumbi walikabiliwa na shtaka la kuiba USD 630,000 (Sh63 milioni) kati ya Agosti 28 2009 na Aprili 5 2016.

Wakurugenzi hao wa benki hiyo ya Chase walikabiliwa na shtaka lingine la kukataa kufuata sheria za benki katika utenda kazi wao kwa kuruhusu ulanguzi wa fedha kuendelea katika benki hiyo kinyume cha sheria kwa kuruhusu wateja wake kujipatia zaidi ya USD ($) 10,000 bila kuiarifu Benki Kuu ya Kenya (CBK).

Bw Miller aliomba mahakama iwaachilie kwa dhamana akisema polisi wamepunguza kiwango cha pesa walichodaiwa waliiba kutoka Sh1.6bilioni hadi Sh529milioni.

Waliachiliwa kwa dhamana ya pesa tasilimu Sh500,000 hadi Julai 12 kesi itakapotajwa

  • Tags

You can share this post!

Washukiwa wa NYS wanyimwa dhamana tena

Niliamuru kufutwa kwa zabuni za Anglo-Leasing – Kinyua

adminleo