Mungatana aomba kesi dhidi yake isuluhishwe nje ya mahakama
Na Richard Munguti
ALIYEKUWA Mbunge wa Garsen Danson Mungatana na mfanyabiashara Paul Collins Waweru watajua hatma yao katika kesi ya ulaghai wa Sh1.96m Jumatano.
Muungatana na Waweru walimsihi hakimu mkuu mahakama ya Kibera Abdulkadir Lorot awaruhusu wasuluhishe kesi hiyo na walalamishi wawili Bi Ann Wairimu Thumi na Bi Cynthia Mukami Kamau.
“Naomba hii mahakama isitishe kushtakiwa kwa Mungatana na Waweru kuwawezesha kusikizana na kusulihisha kesi hii nje ya mahakama,” wakili Lynn Ngugi anayemwakilisha Muungatana aliomba korti.
Bi Ngugi anayemwakilisha Muungatana pamoja na wakili Peter Wena alieleza hakimu ombi lake ni kuambatana na kipingee cha katiba nambari 150 kinachokubalia mizozo kusuluhishwa nje ya mahakama na ” hata kwa njia za kitamanduni ambapo wazee huwapatanisha wanaozozana.”
Ombi hilo liliungwa mkono na wakili anayewakilisha walalmishi Bi Thumi na Bi Kamau.
“Tunagoja pesa zilizotwaliwa na washukiwa hawa ziingie katika akaunti za walalamushi ndipo tutie sahini cheti cha masikizano,” wakili Mabeya anayewakilisha alimweleza
hakimu.
Mahakama ilielzwa tayari mkataba wa kufutulia mbali kesi dhidi Muungatana na Waweru umetayarishwa.
” Mkataba jinsi washtakiwa watakapolipa pesa hizo umetiwa sahini na utakabidhiwa afisi husika;”Bw Lorot alielezwa na mawakili Ngugi na Wena.
Lakini kiongozi wa mashtaka Nancy Kerubo alipinga onbi la kufutiliwa mbali kwa kesi hiyo alisema ‘idara ya majeshi inahusika.”
Bi Kerubo alieleza korti suala hili liko na umuhimu sana kwa umma.
Muungatana na Waweru wamekanusha shtaka kwamba walighyshi cheyi cha mauzo ya bidhaa kwa idara ya majeshi.
Wamedaiwa walipokea kitita cha Sh930000 kutoka kwa Bi Kamau wakidai wangelimsaidia kupata tenda ya kuuzia idara ya kijeshi bidhaa kupitia kampuni yao Beni Trading Ltd.
Hakimu alihoji ikiwa washtakiwa walikuwa na uwezo wa kuondoa kesi dhidi ya wawili hao.