Habari Mseto

Mwalimu kukaa jela miaka 20 kwa kunajisi

June 1st, 2024 Kusoma ni dakika: 1

NA JOSEPH OPENDA

MWALIMU wa zamani katika Shule ya Msingi ya Tembo, atatumikia kifungo cha miaka 20 gerezani kwa kumnajisi mwanafunzi mwenye umri wa miaka 14 baada ya juhudi zake za kuachiliwa huru kugonga mwamba.

David Langat alikamatwa Januari 12, 2019, na kushtakiwa kuhusu kunajisi katika Korti ya Molo baada ya kugunduliwa kwamba mtoto aliyekuwa mwanafunzi wake alikuwa na mimba.

Mahakama ilimpata na hatia Agosti 13, 2020, na kumhukumu kifungo cha miaka miwili jela.

Langat alikata rufaa iliyotupiliwa mbali na Mahakama Kuu mnamo Julai 7, 2021.