• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 8:55 PM
Mwanafunzi afariki kutokana na corona Mumias

Mwanafunzi afariki kutokana na corona Mumias

BENSON AMADALA NA FAUSTINE NGILA

Mwanafunzi wa kidato cha nne wa shule ya upili ya wasichana ya St Elizabeth Lureko Mumias Magahribi  amefariki kutokana na virusi vya corona.

Mwanafunzi huyo alifariki alipokuwa akipokea matibabu kwenye hospitali ya Lifecare Bungoma. Alishuku kwamba alipopata ugonjwa huo aliposafiri kwenda nyumbani.

Kifo cha mwanafunzi huyo kinajiri wakati idadi ya maambukizi shuleni eneo la Magharibi mwa Kenya  imeogezeka kati ya wanafunzi ambao wagoja mtihani wa kitaifa.

Waziri wa afya wa Kaunti ya Kakamega Dkt Collins Matemba alisema kwamba wazazi wa msichana huyo wametibiwa nyumbani kwao Mumia Magharibi.

Wanaaminika kuwa wako salama. Wanafunzi huyo aliripotiwa kusafiri kwenda nyumbani kabla ya kugojeka na akakibizwa hospitali ya St Mary Mumias na baadaye akahamisiwa.

“Tumetuma maafisa wa afya shuleni humo kungalia hali ilivyo na kuweka mikakati ya kuzuia kusambaa Zaidi,”alisema Dkt Matemba.

Katika shule ya upili ya St Peter wanafunzi tisa waketengwa baada ya kupatikana na virusi vya corona.

Wanafunzi watatu kutoka shule hiyo wametengwa kwenye hospitali ya Mumias huku wengine wakiwa kwenye hospitali ya Likuyani. Mwanafunzi mmoja anatibiwa nyumbani.

 Mwanafunzi huyo liyefariki aliripotiwa kusafiri nyumbani akiwa mgonjwa na akakibizwa hospitali ya St Mary Mumias kabla ya kuhamishiwa hospitali ya Lifecare baada ya hali yake kuzorota.

  • Tags

You can share this post!

VIFO: Joho awahimiza wakazi wa Mombasa wazingatie kanuni za...

Waiguru afunga afisi yake sababu ya corona