• Nairobi
  • Last Updated May 1st, 2024 7:02 PM
Mwanafunzi amtetea mwalimu kwenye kesi ya unajisi

Mwanafunzi amtetea mwalimu kwenye kesi ya unajisi

Na Titus Ominde

Mwalimu mmoja wa shule ya msingi ambaye anakabiliwa na mashtaka ya kunajisi mwanafunzi wa darasa la nane alionekana kupata afueni wakati mmoja wa wanafunzi wake alipomtetea dhidi ya mashtaka husika.

Mwanafunzi huyo ambaye ni shahidi wa upande shtakiwa aliambia mahakama kuwa mashtaka dhidi ya mwalimu huyo ni njama ya utawala wa shule.

Akitoa ushahidi wake,aliambia mahakama kuwa wanafunzi wa kike wa darasa la nane walipigwa na kulazimishwa kutoa ushahidi wa uongo dhidi ya mwalimu huyo.

“Naomba niambie hii korti ukweli, hii kesi mwalimu wetu amewekelewa, tulipigwa afisini na kulazimishwa kutoa ushahidi wa uongo dhidi ya mwalimu ili tuseme amekuwa akitunajisi,” alisema mtoto huyo.

Katika kesi hiyo Bw Christopher Kimutai anakabiliwa na mashtaka ya kunajisi mwanafunzi wa darasa la nane katika shule ya msingi ya SUPAS Elite School katika eneo la Sugoi kaunti ndogo ya Turbo kati ya Juni Mosi na Julai 23 mwaka wa 2015.

Akijitetea Bw Kimutai aliambia mahakama kuwa kesi dhidi yake ni propaganda ya kumdunisha kutoana na tafauti kati yake na utawala wa shule.

Ripoti ya uchunguzi wa matibabu kutoka katika hospitali ya mafunzo na rufaa ya Moi MTRH mjini Elodret ilionyesha kuwa mlalamishi hakuwa na majeraha sehemu za siri.

Mshtakiwa aliachiliwa kwa bondi ya Sh100,000.

  • Tags

You can share this post!

2007/8: Wengi waliolipwa fidia baada ya machafuko walikuwa...

Wanahabari huru kuangazia kesi ya ufisadi inayokabili Kenya...

adminleo