• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 8:55 PM
Mwanawe Jenerali Ogolla afichua mali haikumfurisha kichwa CDF

Mwanawe Jenerali Ogolla afichua mali haikumfurisha kichwa CDF

NA MARY WANGARI

MISAFARA ya magari ya kifahari na mali aliviona kama ubatili mtupu, marehemu Jenerali Francis Ogolla, atakayezikwa Jumapili katika kijiji cha Mor, eneobunge la Alego Usonga, Kaunti ya Siaya.

Akinukuu Mathayo 5:3 inayosema ‘heri walio maskini wa roho maana ufalme wa mbinguni ni wao’, Bw Joel Rabuku ambaye ni mwanawe Jenerali Ogolla alimkumbuka babake kama aliyekuwa mtu maskini zaidi rohoni.

“Alielewa kuwa wadhifa wake ulikuwa wa muda tu na ungefika mwisho. Hii misafara mingi, afisi, watu kumwita CDF, Jenerali, kwake havikuwa na maana. Aliviona kama nyenzo tu ya kumwezesha kutekeleza kazi yake,” akasema Bw Rabuku mnamo Jumamosi katika Ulinzi Sports Complex jijini Nairobi.

“Msifikirie kwamba alidhani ni wa maana sana alipovuta pumzi yake ya mwisho,” alisema kijana huyo wa kiume akizungumza katika ibada ya kumpa heshima ya mwisho Jenerali Ogolla aliyeaga dunia Alhamisi pamoja na wanajeshi wengine tisa.

  • Tags

You can share this post!

Barobaro ‘mwelewa shida’ ajitokeza kuwafaa wanafunzi,...

Tanzia: Ex-mume wa Lady JayDee aaga dunia

T L