• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 7:50 PM
Mzazi wa kiume wa mwanawe Anne Thumbi ni marehemu Ken Okoth

Mzazi wa kiume wa mwanawe Anne Thumbi ni marehemu Ken Okoth

Na CHARLES WASONGA

MATOKEO ya uchunguzi wa DNA yamethitisha kuwa baba ya mwanawe diwani maalum wa Nairobi Anne Thumbi, ni aliyekuwa mbunge wa Kibra marehemu Ken Okoth.

Wakili wa diwani huyo Danstan Omari alisema Alhamisi sampuli tatu zilitotolewa kwa maiti ya marehemu kabla ya kuteketezwa zilichunguzwa katika maabara za humu nchini na mataifa ya nje na kuthitisha ukweli huo.

“Taasisi ya Uchunguzi wa Kimatibabu Nchini (Kemri) ilithibitisha kuwa uwezekano wa babake mvulana huyo mwenye umri wa miaka mitano ni asilimia 99.99. Matokeo yalikuwa ni hayo kutokana na sampuli zilizotumwa ng’ambo,” akasema Bw Omari.

Kabla ya mwili wa Okoth kuteketezwa, Bi Thumbi alikuwa amewasilisha kesi kortini kupinga shughuli zozote kama hizo au hata mazishi ya kawaida kabla ya familia ya Okoth kumtambua mtoto huyo na kumshirikisha katika mipango ya kumpumzisha marehemu.

Diwani huyo aliwashtaki mamake Okoth, Angeline Okoth na mkewe Monica Okoth pamoja na hifadhi ya maiti ya Lee.

“Kile nataka ni itambuliwe kuwa babake mtoto wangu ni Ken Okoth na ahusishwe katika matayarisho ya mazishi,” Bi Thumbi akasema kwenye stakabadhi za mashtaka.

Aliandamanisha stakabadhi hizo na picha zilizoonyesha mama Angelina akiwa na mjukuu wake walipokutana wakati mmoja.

Jina la familia

Vilevile, aliwasilisha cheti cha kuzaliwa cha mwanawe kinachoonyesha jina lake la familia kuwa Okoth.

Alhamisi wakili Omari alisema watawasilisha matokeo hayo ya DNA kwa watu wengin wa familia ya marehemu Okoth ambao walikuwa wakishuku madai ya Bi Thumbi.

“Sasa tuna uthibati kwamba mtoto huo ndiye mrithi halali wa mali ya marehemu Okoth,” Bw Omari akasema.

Hii ina maana kuwa mtoto huyo sasa atafaidi kutokana na Sh36 milioni ambazo bunge itatoa kama malipo kwa familia ya marehemu Okoth kulingana na sheria.

  • Tags

You can share this post!

Aliyekuwa Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe afariki

Hekima ya seneti yafungulia magavana mifereji ya fedha

adminleo