• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 11:33 PM
Mzee ambaye nyumba yake iliharibiwa na helikopta ya Rais afidiwa

Mzee ambaye nyumba yake iliharibiwa na helikopta ya Rais afidiwa

Na WINNIE ATIENO

Rais Uhuru Kenyatta hatimaye amemfidia mzee mwenye umri wa miaka 77 ambaye nyumba yake iliharibika wakati ndege ya ujumbe wa Rais ilipotua katika Shule ya Upili ya Kizurini mwaka wa 2017.

Rais ambaye alikuwa ziarani Pwani alitua katika shule hiyo Kaunti ya Kilifi ambapo paa la nyumba ya Mzee James Keah lilisombwa na upepo mkali kutoka kwa ndege hiyo.

Nyumba ya mzee huyo inapakana na shule hiyo. Jiko la shule hiyo pia liliharibika kutokana na upepo unaosababishwa na ndege inapotua au kupaa, hata hivyo hakuna mtu aliumia kutokana na kisa hicho.

Rais alipopokea habari kuhusu nyumba ya mzee Keah, aliagiza ashughulikiwe kuhakikisha nyumba yake inarekebishwa.

Hatimaye alipata msaada baada ya mshirikishi wa eneo la Pwani John Elungata na kamishna wa kaunti ya Kilifi Magu Mutindika kufika katika nyumba yake na kumpa zawadi ya Rais ili arekebishe nymba yake.

“Ninamshukuru Rais Uhuru Kenyatta, singeweza kudhania kuwa ningelipata pesa kama hizi kurekebisha nyumba yangu. Hii ni ishara kuwa Rais anapenda wasiojiweza na wanyonge kama mimi, hii ni heshima kubwa. Sasa nitarekebisha nyumba yangu,” alisema mzee huyo.

Bw Elungata alisema licha ya kuwa msaada huo umechelewa hatimaye umefika.

“Tuko hapa kumpa Bw Keah zawadi ya Rais. Bw Keah ni jirani ya shule ambapo Rais alitua Oktoba 10, 2017. Kwenye ziara ya Rais upepo mkali uliharibu nyumba yake na shule. Tumechelewa lakini muhimu ni kuwa tumefika,” alisema Bw Elungata.

Niabu mwalimu mkuu wa shule hiyo Naomi Kinuhi alisema Sh2 milioni kutoka kwa Rais zimesaidia pakubwa. Jiko la kisasa limejengwa katika shule hiyo.

“Madhari ya shule imebadilika, wanafunzi hawachelewi kwenda kuchukua chakula cha mchana hata msongamano umepungua pakubwa,” alisema Bi Kinuhi.

  • Tags

You can share this post!

Wabunge wa Magharibi watisha kuhama Jubilee baada ya Echesa...

Simanzi yamzidia Kori mkewe Mary Wambui akizikwa kifahari

adminleo