• Nairobi
  • Last Updated May 9th, 2024 6:40 PM
Nampenda mke wangu, tatizo ni kuwa ameniambia hana mpango wa kunizalia

Nampenda mke wangu, tatizo ni kuwa ameniambia hana mpango wa kunizalia

Salamu shangazi. Nina mke ambaye nampenda kwa moyo wangu wote. Tumekuwa katika ndoa kwa miaka miwili sasa na amenishangaza sana kuniambia hana mpango wa kuzaa. Siwezi kuishi bila watoto. Nitakosea kumuacha?

Uamuzi wa mke wako si wa kawaida na sielewi ni kwa nini hakukwambia kabla hujamuoa. Lisilo budi hutendwa. Kama hataki kukuzalia na huwezi kuishi bila watoto itabidi muachane utafute mwingine.

Kwake asali ni lazima…

Kwako shangazi. Ninashuku iwapo mpenzi wangu ananipenda. Sababu ni kwamba akitaka kulamba asali huwa ni lazima hata kama sina hisia hizo wakati huo. Naomba ushauri wako.

Tabia ya mpenzi wako inaonyesha kuwa anajali maslahi yake tu. Na ndiyo maana akitaka huduma hiyo kutoka kwako huwa ni lazima aipate bila kujali hisia zako. Mapenzi ni ushirika wa hiari. Ukihisi huyapati kwake, achana naye utafute mpenzi wa dhati.

Nitakaidi wazazi

Kwako shangazi. Wazazi wangu wamenikataza kuolewa na mwanamume ninayempenda. Nimeamua kukaidi ushauri wao kwa sababu huyo ndiye chaguo la moyo wangu. Waonaje?

Hutamkosea mtu yeyote kwa uamuzi wako huo. Mapenzi na ndoa ni haki na hiari ya mtu binafsi. Wewe ni mtu mzima na una uwezo wa kuamua na kutekeleza jambo lolote kuhusu maisha yako.

Huyu atapindua serikali?

Kwako shangazi. Rafiki yangu amekuwa akimpa lifti mpenzi wangu kwa sababu wanafanya kazi eneo moja mjini. Nina wasiwasi atatumia fursa hiyo kupindua serikali.

Ni kawaida ya maisha kwa watu kubadili nia kuhusu mambo mbalimbali. Mpenzi wako akiamua kukuacha na kumpenda rafiki yako hutamzuia. Tosheka kwamba ni wako kwa sasa.

  • Tags

You can share this post!

Kibali cha mazishi chapasua katikati familia ya mwanasiasa

Mwanamume aliyefaa kupelekwa Marekani kushtakiwa atoroka...

T L