National Bank yafunga matawi kubana matumizi
Na BERNARDINE MUTANU
Benki ya National imefunga baadhi ya matawi katika mkakati mpya wa kupunguza gharama na kukuza mapato.
Benki hiyo ilifunga matawi ambayo hayakuwa yakifanya vyema, alisema meneja wa mawasiliano Patrick Kinyua Jumatano.
Sekta ya benki imekuwa ikikabiliwa na changamoto kubwa ambapo benki nyingi zimewafuta kazi baadhi ya wafanyikazi, hasa kutokana na mazingira magumu ya biashara nchini.
Januari, benki hiyo iliwafuta kazi wafanyikazi 150 kwa lengo la kudhibiti hasara hasa baada ya kupungukiwa na mapato baada ya ushuru hadi Sh138.1 kufikia Septemba 2017, ikilinganishwa na Sh521 milioni kipindi hicho mwaka wa 2016.
Benki zingine pia aidha zimepunguza wafanyikazi na matawi kukabilian na mawimbi katika uchumi nchini.