Obado abambwa baada ya kuhepa polisi
NA Ruth Mbula
Gavana wa Migori Okoth Obado alikamatwa Jumatano baada ya mazungumzo ya saa tatu na maafisa wa EACC mjini Kisii.
Hii ni baada ya kujiwasilisha mbele ya maafisa wa EACC afisi zilizoko kwenye barabara ya Kisii kuelekea Kilgoris baada ya kuhepa kukamatwa kwa madai ya kuiba pesa za umma.
Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umaa Noordin Haji alithibitisha mashtaka dhidi yake pamoja na familia yake Jumanne baada ya kukubaliana na matokeo ya EACC.
“Kila kitu kiko sawa,” Bw Obado aliwaambia wanahabari alipokuwa akitoka afisi za EACC kueleka Nairobi ambapo anatarajiwa kufikishwa mahakamani.
Bw Obado ambaye anatumikia mwaka wake wa pili kwa ofisi yake alifika kwenye ofisi za EACC akiwa ameambatana na wana wake, jamaa zake na pamoja na wasaindizi wake wa ofisi.
Wanahabari, .marafiki na wafuasi wa Obado walifungiwa nje ya afisi za EACC. Baada ya mazungumzo hayo na EACC gavana Obado alikamatwa pamoja na watoto wake wanne.
Watoto hao, Susan Scarlet, Jerry Zachary, Evelyn Adhiambo na Dan Achola Okoth walionekana wajasiri walipokuwa wakisindikizwa na polisi kwenye gari lililowapeleka Nairobi.
TAFSIRI NA FAUSTINE NGILA