• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 8:55 AM
Omanga ashambulia vikali Malala kwa teuzi za ‘kikabila’ chamani UDA

Omanga ashambulia vikali Malala kwa teuzi za ‘kikabila’ chamani UDA

NA LABAAN SHABAAN

ALIYEKUWA Seneta Maalum Millicent Omanga amemkemea vikali Katibu Mkuu wa Chama cha UDA Cleophas Malala baada ya kuteua wanachama wapya wa chama.

Bi Omanga anasema Bw Malala alienda kinyume na matakwa ya wanachama kwa kuteua sekretarieti mpya ya chama hicho tawala.

Shutuma dhidi ya aliyekuwa Seneta wa Kakamega zinamsawiri kupendelea jamaa yake na marafiki ambao Bi Omanga anasema hawakuchangia chochote katika kukuza chama.

“Wanachama waliopigania chama lazima wapate mgao wa haki katika usimamizi wa chama ama kisambaratike; wakati ni sasa!” alisema Omanga kupitia chapisho kwenye akaunti yake ya mtandao wa Facebook.

Msimamo wa Bw Malala unakinzana na mtazamo wa Bi Omanga baada ya kusema mpango huu utafanya UDA kuwa thabiti alipotangaza mabadiliko mnamo Jumatatu Januari 8, 2024.

Katika Ofisi Kuu ya Katibu Mkuu, wanachama watakuwa Alfred Makotsi (Msaidizi Mkuu), Victor Welden (Mshauri wa Kisiasa),  Patience Kiti (Meneja wa Ofisi), Arnold Maliba (Mshauri wa Mikakati ya Mawasiliano), Joseph Akwiri (Meneja wa Mahusiano na Vyombo vya Habari), Betty Truphena Mbogo (Mshauri wa Uhamasishaji wa Rasilimali, Programu na Ushirikiano) na Geoffrey Kipsang (Mkuu wa Mikakati ya Utafiti).

Wengine walioteuliwa ni Ong’wen Justine (Mkuu wa Itifaki) Dominic Chege (Mshauri na Msimamizi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano na Uchaguzi, Wangeci Linar (Mshauri wa Kisheria), Momanyi Brian (Ofisa wa Mawasiliano na Upigaji Picha), Dickson Omari (Ofisa wa Mawasiliano na Video), Lucy Kaleke (Ofisa wa Mawasiliano), Mulusa Evans (Ofisa wa Mawasiliano Dijitali) Catherine Gathoni na Amboye Shakila ambao ni Makatibu Watendaji

Kadhalika, Bw Malala alimpa kazi ya Mkurugenzi Mtendaji Nicodemus Bore huku Edwin Kipkoech akiwa Msaidizi naye Dennis Sadimu akafanywa Meneja wa Ofisi.

Sehemu ya wengine walioteuliwa inajumuisha Samora Machel (Meneja wa Masuala ya Bunge), Sande Oyolo (Meneja wa Ushirikiano na Kaunti), Marvin Orengo (Ofisa wa Mawasiliano), na Hellen Njeri (Katibu Mtendaji).

Bw Malala amekuwa akikashifiwa na viongozi wa vyama tanzu vya Muungano wa Kenya Kwanza kwa kushinikiza kuwepo kwa chama kimoja cha UDA.

Matukio haya yanatarajiwa kuendelea kuibua hisia mseto katika kambi ya chama cha ‘hasla’ hasaa waliokosa kufaidi teuzi katika nyadhifa serikalini na katika orodha ya uongozi wa chama cha UDA ambacho kitafanya uchaguzi mwaka huu.

  • Tags

You can share this post!

Wauguzi waitiwa kazi 2,500 nchini Saudia

Shule yalia matokeo licha ya kuwika Kilifi

T L