• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 9:01 PM
Polisi wachunguza kisa cha mfanyabiashara kuvamiwa

Polisi wachunguza kisa cha mfanyabiashara kuvamiwa

NA DICKENS WASONGA

Polisi wanachunguza kisa kimoja ambapo mwanabiashara kutoka Busia alivamiwa na majambazi waliokuwa wamejihami  nyumbani kwake saa mbili usiku Jumamosi.

Kulingana na ripoti za polisi zilizoonekana na Taifa Leo, Husssein Omondi Mbagai alivamiwa na watu waliokuwa wamejihami nyumbani kwake Sega.

Kamanda wa polisi wa kaunti ya Siaya Francis Kooli alisema mwanaume huyo wa miaka 48 alipigwa na kukatwakatwa na kuachwa na majeraha na hakuna mali yake iliibwa.

“Alikuwa amekatwa shingoni na kichwani. Inasemekana kwamba mmoja wa majambazi hao alikuwa amejihami na bunduki lakini hakuna risasi ilipigwa,” alisema Bw Kooli akiogeza kwamba polisi walikuwa wanawatafuta wahalifu hao.

Mwili wake ulipelekwa kufanyiwa upasuaji hospitali ya Classmate Palour.

Afisa wa DCI kutoka Bondo amekamata washukiwa sita wanaosemekana kuwa walihusika visa vya wizi, kuteka nyara na kubaka.

Genge hilo lilikuwa linadai pesa kutoka kwa familia ya wale walioteka nyara na limekuwa likivamia wafanyakazi wa baa usiku wakienda nyumbani.

TAFSIRI NA FAUSTINE NGILA

  • Tags

You can share this post!

RIZIKI: Maisha yanahitaji mja awe mbunifu

Aliyekuwa mbunge wa Belgut afariki