• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 6:47 PM
Polisi wachunguza kisa cha mwenzao aliyejitia kitanzi

Polisi wachunguza kisa cha mwenzao aliyejitia kitanzi

GEORGE ODIUOR NA FAUSTINE NGILA

Polisi maeneo ya Suba Kaunti ya Homabay wanachunguza kifo cha aliyekuwa afisa wa polisi  anayekisiwa kuwa alijitia kitanzi  kwa kutumia kimbaa cha dirisha.

Afisa huyo wa kitambo Samuel Obote alipatikana akiwa amefariki akiwa ameninginia  na kitambaa ya dirisha kwenye Kijiji cha Onga’o  eneo la Kaksingiri Mashariki.

Mwili wake ulipatikana na mwanawe alipokuwa ameenda kumwamsha baada ya kukosa kuamka masaa yake ya kawaida.

Bw Obote alifanya kazi Kaunti ya Mombasa kabla ya kutolewa kazini miaka chache iliyopita.

Alikuwa anafanya kazi ya usafiri wa umma Kaunti  ya Homabay na mji wa Sindo.

Kulingana na majirani Bw Obote alikuwa na matatizo ya ndoa.Kulingana na Kamanda wa polisi wa kaunti ndogo ya Suba Antony Njeru mwanamume huyo  na mkewe walitengana miezi tatu iliyopita.Majirani wake walisema  kwamba mwanamume huyo alikuwa na msogo wa mawazo kufuatia kutengana na mkewe.

Bw Njeru alisema kwamba uchunguzi unaendelea kubaini kilichotokea.

Mwili wa mwendazake ulipelekwa kwenye chumba cha kuifadhi mkaiti cha Sindo.

  • Tags

You can share this post!

Mgonjwa wa corona aangamia ajalini Taita

Maraga aagiza korti ya Nanyuki ifungwe