• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 12:18 PM
Pombe iliyonaswa yapelekwa kuunda sanitaiza

Pombe iliyonaswa yapelekwa kuunda sanitaiza

NA RICHARD MUNGUTI

Wenye vilabu wawili waliokaidi agizo la Rais Uhuru Kenyatta la kutowauzia walevi pombe walijuta Alhamisi pale walipotozwa viwango vya juu vya faini ama kutumikia vifungo gerezani wakishindwa kulipa faini.

Na wakati huo huo hakimu mkuu Andulkadir Lorot aliamuru kreti za pombe na mvinyo mkali kupelekwa taasisi ya utafiti wa dawa kutengeneza sanitaiza.

“Je, mnajua sababu gani tunaendeleza kesi chini ya miti,” Lorot aliwauliza washtakiwa hao wawili wanawake.

Wakajibu, “Kwa sababu ya Corona.”

Hakimu aliendelea kuwailiza ,” Je mlisikia agizo la Rais Kenyatta Pombe isiuzwe.”

“Ndio tulisikia lakini shida imetusonga.Ilibidi tufungue vilabu tuuze pombe tupate pesa za kujikimu kimaisha ”

Wauzao tembo hao walinweleza hakimy kuwa wako na wagonjwa wanaowashughulikia na hawana pesa za kuwanunulia madawa.

Washtakiwa hao walijitetea zaidi wakiomba mahakama ipitishe ujumbe kwa Rais Kenyatta kwamba wananchi wanaotegemea biashara ya kuuza pombe wameumia na “hawana namna nyingine ya kujipatia fedha za kujisaidia na kununulia watoto vyakula.

Lakini hakimu akawashauri ,” sio lazima uuze pombe upate pesa. Mnaweza uza mboga na matunda.”

Bw Lorot aliwaeleza kuwa siku hizi “mboga zinatembezwa mitaani na hata kuuzwa kwa magari ya kibinafsi.’

Washtakiwa hao waliomba msamaha lakini kiongozi wa mashtaka akaomba waadhibiwe vikali kwa vile amri ya “Rais yapasa kutekelezwa na wote.”

Akiwahukumu Bw Lorot aliwaeleza kuwa “walevi hawana adabu..hawakai umbali unaotakiwa na wizara ya afya ya mita moja unusu ama mita mbili.”

Alisema ugonjwa wa covid-19 unaezwa kwa pupa na wanaokongamana na hata kukumbatiana.

Kila mmoja wa hawa wawili walitozwa faini ya Sh50,000 ama watumikie kifungo cha miezi mitatu gerezani.

Walipewa siku 14 kukata rufaa.

  • Tags

You can share this post!

Kizaazaa polisi wakitaka kumkamata Mungatana kortini

Aagizwa asiseme na mwanamke aliyemtumia picha za uchi