• Nairobi
  • Last Updated May 20th, 2024 6:55 PM
Punda nchini wapungua kwa viwango vya kutisha – ripoti

Punda nchini wapungua kwa viwango vya kutisha – ripoti

Na MAGDALENE WANJA

UTAFITI ambao umefanywa na Shirika la Utafiti wa Kilimo na Mifugo Nchini (Karlo) unaonyesha kuwa punda wako katika hatari ya kuisha nchini kwa muda wa miaka minne ijayo.

Ripoti ya utafiti huo iliyopewa jina ‘Status of Donkey Slaughter in Kenya’ ilikamilika Julai 2019.

Kulingana na ripoti iliyotolewa, ongezeko la mahitaji ya ngozi ya punda hasa nchini China ambako inatumika kutengeneza dawa za kitamaduni, kumechangia katika uchinjaji wa punda aghalabu bila mpangilio katika vijinjio vinne ambavyo vilipewa leseni kati ya 2016 na 2019.

Ripoti hiyo ambayoiliwahusisha washikadau wakiwemo Brooke East Africa na Shirika la Takwimu Nchini (KNBS) ilionyesha kuwa punda waliochinjwa kwa muda wa miaka mitatu iliyopita ni sawa na asilimia 15 ya punda waliosalia kwa sasa.

Utafiti huo unaonyeha kwamba mwaka wa 2016, idadi ya punda waliochinjwa ni 20,768 ambao ni asilimia moja huku mwaka 2017 kukichinjwa punda 12,578 ambayo ni asilimia 6.2 ya punda wote.

Hofu

Mwaka 2018 idadi hiyo ilipanda zaidi hadi 159,631 ambayo ni asilimia 8.1 jambo linalowatia hofu watafiti.

“Licha ya dhana kwamba idadi ya punda itasalia sawa, uchinjaji wa punda kiholela bila kujali jinsia yake kumechangia sana katika kupungua kwa wanyama hao nchini,” lilisema shirika hilo.

Shirika hilo limependekeza kuwa uchinjaji wa punda ufanywe kwa utaratibu huku mipango ya kuzalisha wanyama hIao nchini ikifanyika.

  • Tags

You can share this post!

ANA KWA ANA: Stori yake ni kama telenovela

Mafisadi, baadhi ya asasi zimeishika Kenya mateka –...

adminleo