• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 8:55 PM
Raha kwa madereva wa Uber kupunguziwa bei ya mafuta

Raha kwa madereva wa Uber kupunguziwa bei ya mafuta

Na BERNARDINE MUTANU

Kampuni ya uchukuzi wa teksi ya Uber ikishirikiana na Total Kenya itawapunguzia madereva wake bei ya mafuta na gharama ya kudumisha magari yao.

Ushirika huo ni sehemu ya mpango wa Uber wa kuwatuza madereva wake kwa lengo la kuwasaidia kukuza biashara yao.

“Ushirika huu unalenga kuwapa amani madereva na kuwawezesha kuweka akiba and kuwapunguzia gharama ya kudumisha magari yao,” alisema meneja mkurugenzi wa Uber ukanda wa Afrika Mashariki.

Kulingana na Caroline Abuor Meneja wa Mauzo ya Kadi wa Total Kenya alisema kampuni hiyo itawasaidia kwa kuwauzia mafuta ya kulainisha sehemu zinazosonga za magari yao yaliyo bora zaidi, pamoja na bidhaa zingine za kudumisha magari.

Pia, kampuni hiyo itawapunguzia bei ya mafuta madereva wa Uber kuambatana na mkataba huo.

Pia Uber iliingia katika mkataba wa aina hiyo na kampuni ya bima ya Jubilee kuwapa madereva wake bima bora na wanayoweza kumudu kwa magari yao.

You can share this post!

Lindeni watoto dhidi ya hatari za intaneti – Safaricom

Kampuni zajitokeza kufadhili Beyond Zero

adminleo