Rais wa Senegal awekwa karantini
AFP na FAUSTINE NGILA
Rais wa Senegal Macky Sall aliwekwa kwenye karantini baada ya kutangamana na mgonjwa wa corona lakini alipopimwa hakupatikana na virusi hivyo.
Nchi hio imerekodi visa 6,100 vya corona na vifo 93 kuanzia Mechi.
“Kulingana na ripoti ya daktari rais huyo atajiweka kwenye karantini kwa wiki mbili kuanzia Jumatano ,” alisema Seydou Gueye katika habari aliotoa kwenye televisheni.
Tangu janga hilo kuanza mapema mwaka huu viongozi tofauti wamepatikana na ugonjwa huo akiwemo waziri mkuu wa wa Uingereza Boris John aliyelazwa hospitalini na akapona.