• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 7:02 PM
Ruto amteua dadake Raila kuwa naibu mkuu wa ubalozi mdogo

Ruto amteua dadake Raila kuwa naibu mkuu wa ubalozi mdogo

NA CHARLES WASONGA

UKURUBA wa kisiasa kati ya Rais William Ruto na kiongozi wa Azimio La Umoja-One Kenya Raila Odinga, umeanza kuzaa matunda kufuatia uteuzi wa dadake kiongozi huyo wa upinzani kuwa balozi.

Dkt Akinyi Walkowa ni miongoni mwa wanawake 16 ambao Ijumaa walitunukiwa nyadhifa za ubalozi na unaibu balozi wa Kenya katika mataifa mbalimbali ya kigeni.

Bi Akinyi aliteuliwa kuwa naibu balozi wa Kenya jijini Los Angeles katika jimbo la California nchini Amerika ambapo atahudumu chini ya Ezra Chiloba ambaye aliteuliwa Mkuu wa Ubalozi huo mdogo.

Wanawake wengine waliotunukiwa kuwa mabalozi ni pamoja na Catherine Kirumba Karemu (London, Uingereza), Lilian Tomitom (Lusaka, Zambia) Caroline Kamende Daudi (Ottawa, Canada), Profesa Anne Kisaka Nanguli (Dakar, Senegal), Jessica Muthoni Gakinya (Rabat, Morocco), Halima Yussuf Mucheke (The Hague, Uholanzi), Everylyne Mwenda Karisa (Havana, Cuba), Grace Atieno Okara (UN Habitat) miongoni mwa wengine.

Akizungumza Ijumaa, Dkt Ruto alisema uteuzi huo ni wa kuheshimu mchango wa wanawake katika uongozi wa nchi.

“Leo asubuhi (Ijumaa) niliwateua wanawake 10 zaidi kuwa mabalozi katika sehemu mbalimbali za dunia na manaibu mabalozi wengine sita kwa kutambua mchango wa wanawake katika uongozi,” Dkt Ruto alisema.

  • Tags

You can share this post!

Walimu wasio na kazi wasubiri TSC itangaze nafasi 20,000

Ugumu wa kupambana na wezi wa mananasi Del Monte

T L