• Nairobi
  • Last Updated April 28th, 2024 3:31 PM
Sababu ya kinara wa UNEP kujiuzulu

Sababu ya kinara wa UNEP kujiuzulu

Na BERNARDINE MUTANU

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Mazingira (UNEP) Erik Solheim amejiuzulu.

Solheim aliondoka kwa wadhifa huo Alhamisi, Novemba 22, 2018.

Alichukua hatua hiyo baada ya ripoti ya mwisho ya uchunguzi kuhusu ziara rasmi katika afisi ya usimamizi wa huduma za ndani.

“Saa chache zilizopita, kwa moyo wa huzuni, nimefahamisha Katibu Mkuu wa UN (António Guterres) kuhusiana na uamuzi wangu. Ameashiria kuwa atamteua msimamiz mwingine katika muda mfupi,” alisema msimamizi huyo anayeondoka.

Kulingana naye, ni matumaini yake kwamba hatua yake itakuwa ya manufaa kwa UNEP kuambatana na lengo lake la kukabiliana na changamoto za karne ya 21.

Bw  Solheim, ambaye alichukua mahali pake Achim Steiner kama mkuurugenzi mkuu wa shirika hilo alianza kukosolewa chini ya miaka miwili baada ya kuchukua wadhifa huo.

Ukosoaji huo ulitokana na madai kwamba alitumia mamilioni ya fedha katika ziara zisizo muhimu kulingana na rasimu ya kwanza ya ripoti ya uchunguzi kuhusiana na ziara hizo.

Afisi za UNEP huwa Nairobi, eneo la Gigiri.

  • Tags

You can share this post!

Mwanamume kuozea jela miaka 5,000 kwa mauaji ya halaiki

Serikali yaagizwa kuwalipa wanakandarasi wote

adminleo